MENEJA wa Manchester City Pep Guardiola amesema uzito wa mechi ya leo ya Premier League dhidi ya Chelsea ni zaidi ya fainali.
Timu hizi mbili zilikutana wiki mbili zilizopita kwenye fainali ya kombe la Carabao na Guadiola ameona namna kikosi cha mpinzani wake namna kilivyo.
"Ni fainali kwetu, tunapaswa tucheze kwa kila njia manaa tunakutana na Chelsea kwenye mchezo wetu.
"Wana nafasi ya kuwa mabingwa wa ligi hata kama watu hawaamini kuhusu jambo hili. Wana viungo ambao ni bora ulimwenguni, mlinda mlango mzuri na mabeki wenye uzoefu," amesema.
Safu ya ushambuliaji ya Manchester City iliyo chini ya Sergio Arguero inatisha ndani ya Premier League mwenye mabao 14.
0 COMMENTS:
Post a Comment