February 12, 2019





Mabosi wa Simba wameweka bayana kwamba kwa sasa wanasubiri majibu kutoka kwa viongozi wa timu ya AFC Eskilstuna ili kujua hatima ya kiungo wao, Said Ndemla.

Ndemla kwa wiki mbili sasa aliondoka ndani ya kikosi hicho na kuelekea Sweden kwa ajili ya kufanya majaribio ndani ya kikosi cha Esklistuna ambacho Mtanzania Thomas Ulimwengu aliwahi kukichezea.

Mratibu wa Simba, Abbas Ally amesema wanawasubiri viongozi hao wa AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini humo, wawatumie majibu ya Ndemla kisha ndiyo wajue wanachukua maamuzi gani juu ya kiungo huyo.

“Kwa sasa kikubwa kinachosubiriwa ni majibu kutoka kwa wenzetu AFC Eskilstuna baada ya Ndemla kwenda huko na kurudi hapa nchini.

“Sisi hatujui chochote kilichotokea kwenye majaribio yake zaidi ya wao ambao ndiyo wana majibu kamili, wakishatuma majibu ndiyo viongozi wataamua sasa juu yake,” alisema Abbas.

3 COMMENTS:

  1. Wewe ndio unamgeuza Manara awe ishu namba moja.Hakuna cha kujadili?Uongozi wa Simba umeshazungumzia suala lake.
    Wakati mwingine ni bora kutoandika lolote kuliko kuandika makala ndefuuuu isiyo na mbele wala nyuma.

    ReplyDelete
  2. Hapa inaonesha ni nyota wachezaji wa Simba ndio wanaovutia vilabu vya nje na si wengineo

    ReplyDelete
  3. Basi watowe ripoti wamekaa tu kimya kumbe hata wazungu wapo waafrika du!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic