Vinara wa Ligi Kuu Bara Yanga, tayari wako kambini mjini Morogoro. Kikosi hicho kimetua Morogoro jana.
Wakati Simba wanashuka dimbani leo kuwavaa Al Ahly, Yanga wameanza kambi rasmi kuiwinda Simba katik mechi ya Ligi Kuu Bara, Jumamosi.
Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu kubwa kwa kuwa kila timu itataka kushinda kwa hesabu za ligi kuu.
Kama Yanga itashinda mechi hiyo itajiweka katika nafasi nzuri ya ubingwa.
Simba nao wanataka kushinda ili kuitikisa Yanga lakini kuhakikisha wanakuwa na mwendo mzuri wa mechi zao rundo za viporo.
0 COMMENTS:
Post a Comment