UONGOZI wa Namungo FC, umesema kuwa kwa sasa wanaiweka kando timu ya Yanga badala yake wanawekeza nguvu kubwa kwenye mechi zao za Ligi Daraja la Kwanza.
Namungo yenye ngome yake mkoani Mtwara itacheza na Yanga katika mchezo wa kombe la Shirikisho ikiwa ni hatua ya 16 bora kati ya Februari 21 au 23 Uwanja wa Majaliwa.
Ofisa Habari wa Namungo, Kidamba Namlia amesema kikosi chao kipo imara kushiriki mashindano yote ila kwa muda tu wanaiweka kando Yanga.
"Tunajua tuna mchezo na Yanga ambao upo mbele yetu, kwa sasa hatuna presha nao bali tunaweka nguvu kubwa kwenye michezo yetu ya Ligi Daraja la Kwanza ambayo tupo nayo kwa sasa.
"Tutaanza na Mbeya Kwanza, Uwanja wa Sokoine kisha tutacheza na Mufindi watakuja Uwanja wa Majaliwa baada ya kuzimaliza hizi mechi ngumu tutaanza kuiwinda Yanga," amesema Namlia.
0 COMMENTS:
Post a Comment