February 8, 2019


MSHAMBULIAJI wa Mtibwa Sugar, Jaffary Kibaya amewafanyia ubaya African Lyon leo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Manungu, Morogoro baada ya kusawazisha bao dakika za lala salama.

Katika mchezo wa leo, African Lyon walianza kupata bao dakika ya 61 kupitia kwa Ramadhan Chombo na wakaamini kwamba watabeba pointi tatu ugenini.

Dakika za lala salama, Jaffary Kibaya alifunga bao na kusawazishia timu yake ya Mtibwa Sugar ndani ya dakika mbili za nyongeza, hali iliyopelekea matokeo kuwa 1-1, huku Kibaya akiwafanyia ubaya mara ya pili kwani mzunguko wa kwanza aliwatungua mabao mawili Uwanja wa Uhuru.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic