RASMI ZAHERA ATOA NAFASI KWA JEMBE JIPYA YANGA
KIUNGO mchezeshaji mpya wa Yanga, Mohammed Issa ‘Banka’, rasmi anatarajiwa kuonekana uwanjani keshokutwa Jumapili hii katika mchezo wa Ligi Kuu Bara baada ya kumaliza adhabu yake ya kifungo.
Banka alifungiwa na Kamati ya Kuzuia na Kupambana na Dawa Zisizoruhusiwa Michezoni ya Kanda ya Tano Afrika (RADO) ambayo ilitoa hukumu ya kumfungia mwaka mmoja baada ya kugundulika kwenye michuano ya Cecafa.
Kiungo huyo aliyesajiliwa na Yanga kwenye msimu huu wa ligi akitokea Mtibwa Sugar, leo Alhamisi rasmi adhabu inamalizika huku akitarajiwa kuanza kuvalia jezi ya kijani na njano katika mchezo ujao wa ligi timu hiyo itakapocheza dhidi ya JKT Tanzania, Mkwakwani, Tanga.
Mratibu wa Simba, Hafidh Saleh, alisema kiungo huyo rasmi ataonekana uwanjani katika mchezo unaofuatia wa ligi dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Saleh alisema kiungo huyo muda mrefu alikuwa tayari ameingiziwa mfumo na programu za Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera katika mazoezi yake ya kila siku aliyokuwa anawafanyisha wachezaji wake.
“Rasmi Banka adhabu yake inatarajiwa kumalizika kesho (leo), hivyo mashabiki watarajie kumuona uwanjani katika michezo ijayo ya ligi kwa kuanzia huu unaofuata dhidi ya JKT Tanzania.
“Adhabu ya Banka imemalizika katika kipindi kizuri ambacho timu inamhitaji, kama unavyoona ratiba ilivyotubana ya ligi, wachezaji tunacheza mechi hiyo keshokutwa tunacheza nyingine huku tukisafiri mwendo mrefu,” alisema Saleh.
Uwe makin unapoandika hatuna mratibu wa simba kwenye klabu ya Yanga unatuchanganya isitoshe ww ni mwandish mkubwa wa habar za michezo tz
ReplyDeleteKweli kabisa hata mimi nimeshangaa
ReplyDeleteAtutaki vitu vyako vya simba yanga mratibu analipwa yanga
ReplyDeleteAchaaa ushamba mapenzi unayaleta had kwenye kaz yako tunajua km unaipenda simba
ReplyDelete