February 6, 2019


Bodi ya Wakurugenzi Simba ikiongozwa na Mwekezaji Mkuu, Mohammed Dewji 'Mo', leo imekutana kujadili mambo mbalimbali ya klabu hiyo.

Katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam, inaelezwa yaliyozungumzwa ni kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly na mechi za Ligi Kuu.

Taarifa zilizo chini ya kapeti zinasema ni kuwa Bodi hiyo imejadili kwa kina mkakati mzima wa kuhakikisha Simba inashinda mechi hiyo ili kujiwekea inafanikiwa kujiwekea mazingira mazuri ya kufika hatua ya robo fainali.

Aidha, bodi hiyo imegusia pia namna ya kuhakikisha Simba inazidi kuwa mwakilishi mwakani wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuchukua ubingwa wa ligi msimu huu.

Simba itakuwa na kibarua kesho dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa taifa Dar es Salaam ambapo mechi itaanza majira ya saa 1 za usiku.

2 COMMENTS:

  1. Bodi ya yenye Mwekezaji mmoja mwenye hisa pekee duu

    ReplyDelete
    Replies
    1. usiwe na shaka wenye hisa mda si mrefu watakuwa wengi. mie mwenyewe nimepanga kununua hisa pindi wakianza kuuza kwa wanachama!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic