BEKI kiraka wa timu ya Manchester City, Danilo Luiz da Silva amesema sare ya Liverpool mbele ya WestHam imewapa hamasa wachezaji wenzake.
Danilo amesema ameshangazwa na Liverpool kushindwa kupata matokeo kwenye Uwanja wa London hali inayowapa fursa wao kurejesha heshima kwenye mchezo wao dhidi ya Everton.
Amesema :"Ni nzuri kwetu na kila mmoja ndani ya chumba cha kubadilishia nguo kujua kuhusu hilo, ila kama hatutafanya kazi yetu ipasavyo haitoshi. Hivyo furaha yetu itakamilika pale tutakapofanya kazi kubwa.
"Ilikuwa balaa kwetu kuacha pointi kwa Newscastel, lakini msimu huu ni mrefu. Tuna michezo mingi ya kucheza. Liverpool wanafanya vizuri kama nasi tutaendelea kushinda tutakua sehemu nzuri,".
0 COMMENTS:
Post a Comment