February 11, 2019


FEBRUARI 16, mwaka huu kwenye goli la Yanga atakaa Klaus Kindoki au Ramadhan Kabwili hii ni baada ya Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kusema hatamrudisha kipa wake, Beno Kakolanya licha ya baadhi ya mashabiki kumtaka amrudishe kwa ajili ya mechi hiyo ya Simba.

Kakolanya amekuwa nje ya kikosi cha Yanga baada ya kuibuka kwa sintofahamu kati yake na uongozi wa timu hiyo kuhusiana na maslahi yake. Kwa sasa Zahera amekuwa akiwatumia makipa Ramadhan Kabwili na Klaus Kindoki.


Kakolanya alikuwa na mchango mkubwa ndani ya Yanga kwenye mechi ya kwanza mbele ya Simba kwa kutoruhusu bao licha ya kushambuliwa mara nyingi na mechi hiyo kumalizika kwa suluhu. Timu hizo zitakutana tena Februari 16, mwaka huu.

Kocha huyo raia wa DR Congo, amesema kwamba hawezi kumjumuisha kipa huyo kutokana na yeye kuomba kuondoka ndani ya Yanga kwa kutaka kuvunjiwa mkataba wake.

“Watu wanataka nimrudishe Beno kwa ajili ya mechi ya Simba lakini niwaambie kwamba haitawezekana kwa sababu ya vitu vilivyotokea nyuma.

“Yeye mwenyewe ndiye ambaye aliomba aachwe na Yanga kwa kuandika barua sasa nawezaje kumrudisha mtu ambaye ameomba kuondoka ndani ya timu, nitawatumia wachezaji wangu niliokuwa nao kwenye mechi zilizopita,” amesema Mkongomani huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic