February 11, 2019


MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, Meddie Kagere amesema kuwa kwa sasa kikosi chao kina kazi ya kutafuta matokeo chanya kwenye mchezo wao wa kesho (Caf).

Simba ni mabingwa watetezi na kwenye michuano ya kimataifa wanashika nafasi ya tatu wakiwa kundi D baada ya kucheza michezo mitatu na kushinda mchezo mmoja huku ile ya ugenini wakivuruda kwa kuchapwa mabao jumla ya mabao 10.

Kesho Simba watakuwa kibaruani kumenyana na Al Ahly ukiwa ni mchezo wa marudio baada ya ule wa awali uliochezwa Misri uliosha kwa Simba kupoteza kwa mabao 5-0.

Kagere amesema kwama wao waliwafunga kwao basi nao pia wanaweza kupata matokeo kwenye mchezo wao wa marudio.

"Tulifungwa kwao ni muda wetu kushinda nyumbani, tutapambana ili kupata matokeo katika uwanja wetu wa nyumbani," amesema Kagere.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic