MENEJA wa Chelsea, Maurizio Sarri amesema hajaitwa na mmiliki wa kikosi hicho Roman Abramovich kuongea naye kuhusu mustakabali wa kikosi hicho.
Jana Chelasea ilipoteza mbele ya Manchester City kwa kupigwa mabao 6-0 kwenye Uwanja wa Etihad hali iliyoua matumaini ya kumaliza msimu ikiwa ndani ya nne bora alipoulizwa kama anafikiri maongeziyake na mmiliki juu ya nafasi yake, amesema bado hajaulizwa.
"Kama Raisi ataniita nitakuwa na furaha ya kumuona na kusikia kile ambacho hajawahi kuniambia, kiukweli bado sijajua ni namna gani itakuwa.
Chelsea imepoteza michezo yake mitatu ndani ya Premier League ya ugenini, imeruhusu mabao 12 haijafunga hata bao, kwenye kikao na waandishi wa habari, Sarri alisema kuhusu hatma yake ndani ya timu ni maamuzi ya bodi ya uongozi.
Matokeo hayo yanaifanya Chelsea iwe nafasi ya sita kwenye msimamo akishushwa na Arsenal nafasi ya tano kwa tofauti ya mabao ya kufunga licha ya wote kuwa na pointi 50.
0 COMMENTS:
Post a Comment