February 11, 2019







Aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura amesomewa mashitaka 17 mawili yakiwa ya utakatishaji fedha.

Mashitaka hayo yamesomwa leo kwenye Mahakama ya Kisutu baada ya Wambura kupandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza.

Shitaka la kwanza lilikuwa ni kugushi nyaraka wakati akiwa madarakani TFF na kujiwezesha kupata fedha dola 30,000 isivyo halali.

Wambura amekosa dhamana na amepelekwa rumande hadi Februari 14 atakaporejea mahakamani kuendelea na kesi yake ambayo itajulikana iwe ya jinai au uhujumu uchumi.


4 COMMENTS:

  1. Kwakweli ukisikia mtu anaandamwa na mitihani kwa kile anachodhamiria kukifanya basi wambura inatosha tena. Ila ni vizuri tu kusikia wambura ameachana na azma yake ya kuwa moja kati ya kiongozi wa juu wa michezo nchini. Kwanza kufungiwa na FIFA ni hekima za FIFA kuiepusha Tanzania kujiingiza kwenye mgogoro wa uongozi wa chama cha mpira Tanzania wakati huu ikielekea kuandaa Afcon ya vijana .Mabishano yake na Karia yalikua hayana Afya kwa mustakabali wa mpira wa Tanzania kama vile kauli ya utundu Lisu ya Karia unaona jinsi ilivyoleta taharuki kwenye jamii.
    Lakini tukirudi kwa Tundu?Lisu yule mtu sijui kama ni mzima wa akili. Moja kati ya kauli zake nyingi za kuipaka kinyesi Tanzania Duniani Tundu Lisu ameitangazia Dunia rasmi kuwa Tanzania ni, A LAND OF HORROR.yaani Tanzania ni Taifa lisilokuwa salama kwa maisha ya mwanadamu ni nchi ya kuogopwa kwa maovu pengine kwa maoni yake hata Libya ipo salama kuliko Tanzania? Kwa kweli uharibifu anaoufanya Lisu kwa Taifa ulimwenguni ni mkubwa umeshavuka mipaka ya Usaliti. Wakati mwengine kama taifa inabidi kuchukua maamuzi magumu bila ya kujali mataifa mengine yatasema nini kwa raia wake wanaofanya jitihada za kuliangamiza taifa lao wenyewe. Tanzania ni nchi poa la sivyo kwa nchi nyengine Tundu Lisu angesharudi kwa sanduku alipotokea zamani sana. Nchi yetu ni nchi ya sheria lakini licha yakuwa Lisu ni mwanasheria ameamua kwa makusudi kujivisha ujaji yeye mwenyewe na kutoa maamuzi ya kesi yake yeye mwenyewe Anachoendelea kukifanya Lisu kwa sheria za nchi yetu ni dhahiri ni kosa ni kulihujumu taifa. Kwa jinsi Lisu anavyotoa matamshi makali na ya dharu juu ya kiongozi mkuu wa nchi pamoja na taifa ni dhahiri kabisa yakuwa anaendesha kampeni ya kuhamasisha ujasi nchini kwa kiongozi aliechaguliwa kisheria. Kauli za Lisu za raisi wa Tanzania ni sawa na mnyama aneinuka na anafaa kukimbiwa ni kauli za kuwakashifu watanzania wote. Lisu atakuwa anatumiwa aidha yeye mwenyewe anaelewa hilo au la. Kama mtanzania mwenye uchungu na nchi yangu ningeiomba serikali kusimama kidete juu ya hili. Najuwa kuna watu smart zaidi serikalini wa kulishughulikia suala la Lisu kitaalam zaidi, ila wakati mwengine wahusika wanatakiwa kuwa sharp zaidi katika kudili na watu kama akina Tundu Lisu kabla hawajaliletea taifa aibu . Hata hivyo ni vizuri kuwafahamu wale wote waliopo gizani, nyuma ya Lisu wanaomtumia. Mtu au taifa haliwezi kutumia tukio moja la Lisu kujifanya kuwa wana uchungu na demokrasia ya nchi yetu kwakuwa anaipenda sana Tanzania kwa kumfadhili mtu kuipaka matope nchi yetu wakati kuna mengi mazuri yamefanywa Tanzania hakuna alieuliza kwa mfano sidhani wamerican wanaruhusu muislam kuwa raisi wao wa nchi ni nchi namba moja ya demokrasia duniani hiyo. Kila nchi ina taratibu zake na sio vizuri kuzibeza
    Ukitizama utaona kabisa ni vita ya kiuchumi zidi ya Tanzania hasa kuiangamiza sekta yake ya utalii kimataifa na Lisu kazi ya kuiangamiza sekta hiyo ya utalii wa Tanzania anaifanya vizuri kwa ustadi wake wote. Sasa lazima kuwe na kaunta attack ya kujibu mashambulizi hayo ya kifisadi juu ya nchi yetu. Moja ya mambo ya haraka ya kufanya kwa maoni yangu ni kumtumia au kuingia gharama kumtafuta a well known outspoken African scholar with full commanding in English language skills and swahili if possible to step every step where Lisu stepped to rebuke his lies, ni vizuri asiwe mtanzania, having full Magufuli documentary with video if possible to explain the world of how in three years Magufuli is changing Tanzania for the better of his people. Licha ya kutumiwa Lisu peke yake hawezi akawa juu ya Tanzania lazima Dunia ielewe ukweli,watanzania lazima tuamke na hila za nje za kuivuruga nchi yetu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa hii inahusiano gani na taarifa ya juu hapo

      Delete
  2. Hakuna tujualo katika vita hii tuwaachie wenyewe tusijechuma dhambi bure

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic