Ukiachana na wachezaji wanne ambao ni Emmanuel Okwi, Meddie Kagere, Clatous Chama na James Kotei, hii ndiyo orodha ya wachezaji wengine wa Simba ambao hawana uhakika wa kuendelea kuichezea timu, imeelezwa.
Taarifa imeeleza kuwa beki Mganda, Juuko Murushid, Nicolous Gyan, Asante Kwasi na Haruna Niyonzima hawataendelea kuwepo ndani ya Simba na vilevile mikataba yao inamalizika msimu huu.
Wakati huohuo mchezaji kutoka Burkina Faso, Zana Coulibaly na beki Pascal Wawa kutoka Ivory Coast wana uwezekano mkubwa wa kusitishiwa mikataba yao.
Imeelezwa maamuzi hayo magumu ya Simba yanakuja kufanyika ili kuandaa kikosi cha nguvu ikiwemo kusajili wachezaji wenye uhakika wa kuipa timu alama tatu na si wale wa majaribio.
Maamuzi haya pia yamechagizwa na aibu ya vichapo vya mabao matano mara mbili mfululizo katika Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita ya Congo na Al Ahly ya Misri.
Mbali na kuachana na idadi tajwa hapo juu, imeelezwa uongozi umesema utaendelea kuwa na wachezaji ambao wataonesha kubadilika kwa kujituma uwanjani lakini bila hivyo itakuwa ndiyo safari ya kuondoka moja kwa moja.
Usiharibu concentration ya timu kuelekea mechi zero ngumi Achana kuandika gossip unashusha heshima yako saleh jembe
ReplyDeleteZetu ngumu
ReplyDeleteWEWE KWELI TATIZO HUNA HATA UZALENDO WAKATI HUU SIO WA KUWAVURUGA WACHEZAJI WA SIMBA WANAOTARAJIA KUPAMBANA KESHO TU NA WAARABU USISAHAU SIMBA WANAWAKILISHA TAIFA LETU LA TANZANIA
ReplyDelete