February 10, 2019


Baada ya kikao cha Mwekezaji Mkuu wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'Mo' na Bodi ya Wakurugenzi kumalizika siku chache zilizopita, inaelezwa kuwa kuna uwezekano wa kikosi cha timu ya Simba kupanguliwa.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinasema uongozi umedhamiria kufanya usajili wa maana ili kuendana na kasi ya mashindanio ya kimataifa ambayo yanahitaji wachezaji wenye uwezo ansi lelemama.

Sasa, zilizo chini ya kapeti zinasema kuna baadhi ya wachezaji ambao wana uhakika wa kusalia katika kikosi cha kwanza ambao ni wa kimataifa na wengine wakiondoshwa.

Imeelezwa wachezaji Emmanuel Okwi, Meddie Kagere, Clatous Chama na James Kotei ndiyo pekee wa kimataifa walio na uhakika wa kusalia kikosini msimu huu.

Wengine ambao bado wana mikataba na uongozi haujaridhishwa nao wanaweza kuwavunjiwa kisha klabu itafanya usajili mwingine kuendana na matakwa ya mashindano ya kimataifa.

3 COMMENTS:

  1. 💇💇💇💇💇💇

    ReplyDelete
  2. Hata kocha nae aende.

    ReplyDelete
  3. Unamlipa wewe?
    Kocha hana kosa kwa uwezo wa wachezaji waliopo?
    Bodi imekaa imegundua baadhi ya wachezaji ndio tatizo.
    Wewe na ujuaji wako huku huchangii lolote unataka kocha afukuzwe!
    Klabu ikifukuza makocha mnalalamika wakipewa muda ili wale stability ya muda mrefu mnalalamika.
    Hakuna shortcut kwenye mafanikio lazima yapate muda mrefu kuleta mabadiliko ya maana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic