February 21, 2019


Kocha Mkuu wa klabu ya KMC, Ettiene Ndayiragije amesema nia yake ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na timu hiyo. 

Ndayiragije amesema Simba, Yanga na Azam ndiyo washindani wake kwenye mbio za ubingwa msimu huu. 

Kocha huyo anaamini kwa namna wanavyojituma kujiandaa na mechi zijazo za ligi ana imani anaweza akafanya vizuri na kutimiza ndoto zake uwanjani.

Ameeleza kuwa kwa sasa ana timu tatu pekee za kushindana nazo ambazo ni Simba, Yanga na Azam na si zingine ambazo anaamini atazimudu kirahisi.

"Lengo na nia yangu ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, kuna timu tatu pekee ambazo zinanipa ushindani ambazo ni Yanga, Simba na Azam FC na si zingine" amesema.

1 COMMENTS:

  1. Duh hatari sana 😅😅,,jumla timu inatakiwa icheze mechi 38 na ikusanye pointi 114 ila hao KMC wamecheza mechi 27 wamebakiza mechi 11 ambazo ikitokea kashinda zote atafikisha Point 73..ambayo yanga anaeongoza ligi anaeza akazifikia na kuzipita kwa kupata sare michezo yote iliyobakia,,,kitu ambacho si rahisi sababu atashinda tuu..kuhusu simba Kocha WA KMC asubiri tuu maana kwa sasa ndo timu bora msimu huu so awe ana piga hesabu kabla ya kuongea...huu ni mpira sio siasa..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic