February 21, 2019


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ametoboa siri ya ushindi wa timu yake dhidi ya Mbao FC katika Uwanja wa CCM Kirumba jana.

Katika mchezo huo Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuvunja rekodi ya kutokushinda ndani ya Uwanja hu.

Kocha huyo ameeleza kuwa aliwaambia wachezaji wake kama wanaamini wanaenda kushinda basi wapande gari.

Aidha alieleza pia mambo ya kufungwa na Mbao kila siku yatakuwa yamefikia mwisho na ndiyo wakapata matokeo jana.

Niliwaambia wachezaji wangu yeyote anayeamini tunakwenda kushinda mchezo dhidi ya Mbao FC apande kwenye gari, nilisema haya mambo ya kufungwa na Mbao kila wakati leo ndiyo mwisho"

2 COMMENTS:

  1. MWALIMU SI UNGESEMA HIVYO HIVYO BASI TULIPOCHEZA NA SIMBA UMESAHAU KUSEMA WAMETUFUNGA. UJE KUSEMA TUTAPOCHEZA NA AZAM USISAHAU

    ReplyDelete
  2. Bora mumkumbushe ninyi. Safari hii hajawalaumu waamuzi wa Tanzania, Cjui ile mechi na Mbao wamechezeshwa na waamuzi kutoka Kongo! Maana hajagusia kabisa kuhusu waamuzi!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic