KUHUSU UWANJA WA SIMBA BUNJU, MO AJANA TAMKO RASMI
Mwekezaji Mkuu wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji Mo, amewajulisha wapenzi na mashabiki wa Simba kukamilisha zoezi la ujenzi wa Uwanja wa mazoezi Bunju baada ya mwezi mmoja.
Mo amesema kinachofanyika hivi sasa ni harakati za kuzungumza na serikali ili waweze kuchukua nyasi zao ambazo zipo bandarini kwa muda mrefu na zoezi la uwanja liendelee.
Mwekezaji huyo ameeleza endapo nyasi zitachukuliwa basi ujenzi utaenda haraka na Simba inaweza ikaanza kutumia uwanja wake badala ya Bocco Vetrani ambapo kufanyia mazoezi yake kila siku.
Kauli ya Mo imeonesha dhahiri shahiri kuwa nyasi hizo zilisababisha kusimama kwa ujenzi wa uwanja huo na kuepelekea ukimya ambao ulikuwa hauna majawabu.
Na baada ya malalamiko na maswali mengi juu ya uwanja kutoka kwa wadau wa klabu hiyo, Mo ameamua kuweka kila kitu wazi ili kuwajuza wapenzi wa timu hiyo kipi kinachoendelea.
0 COMMENTS:
Post a Comment