ZUNGU AITAKA SERIKALI KUUTAZAMA UWANJA WA SINGIDA, AIONEA HURUMA YANGA
Na George Mganga
Mbunge wa Jimbo la Ilala, Dar es Salaam, Mussa Azzan Zungu, ameitaka serikali kuvifanyia marekebisho viwanja haswa vya mikoani ili kuzipa wepesi timu kushindana vizuri.
Kauli ya Zungu imekuja kufuatia timu ya Yanga kwenda suluhu dhidi ya Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa wiki hii mjini Singida.
Zungu ameutaja Uwanja huo ambao ulitumika kuwa na mapungufu mengi ikiwemo PICHI yake kuwa na matatizo na akiamini ilisababisha matokeo kutokuwa kama ilivyopaswa.
Ameeleza kuwa aliionea huruma Yanga kucheza mechi yake katika Uwanja kama ule ambao uliwapa wakati mgumu kupata matokeo.
Kutokana na changamoto hiyo, Zungu ameitaka serikali ambayo inamiliki viwanja vingi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuangalia namna ya kuvifanyia maboresho ili viendane na hadhi ya Ligi Kuu Bara.
"Kwa Uwanja kama ule kwa Yanga kuchezea ni aibu, hauendani na hadhi ya ligi yetu, naiomba serikali kupitia CCM ifanye namna ili maboresho yafanyike haraka na timu zicheze vizuri" alisema.
Kila kitu serikali,kila kitu serikali,kila kitu serikali.kila kitu serikali kuu. Lakini saidi Baharesa mmoja anamiliki uwanja wa heshima wa kuchezea mpira na huduma nyengine zinazohusiana na mchezo wa mpira. Mkoa mzima unashindwa kuwa na watu wanaoweza ufanikishaji wakuwa na kiwanja angalau sehemu ya kuchezea kuwa salama? Kama kuna taasisi inamiliki kiwanja hicho kwnaini wanashindwa kutimiza wajibu wao wa kuvitunza? Au ni sawa na mwenye ng'ombe anaemkamua maziwa tu bila ya kumpatia malisho? Kila mtu na maono yake ila kwangu mimi serikali za mikoa kushindwa kusimamia hata mambo madogo madogo mpaka kungojea serikali kuu huwa yananitia kichefuchefu na kwa kweli ni miongoni mwa mambo yanayotuchewesha kuendelea watanzania .
ReplyDelete