KWA REKODI HIZI YANGA WANAZOA POINTI TATU
MASHABIKI wa Simba wana uhakika mkubwa kwamba baada ya kuwakosa Yanga kwenye mechi ya kwanza waliyokutana basi safari hii Februari 16, watafanya kweli kwa kutoa mkong’oto.
Wakati mashabiki hao wakiwa na uhakika huo mkubwa rekodi zinasema kwamba wajiandae kisaikolojia kwani kwa mujibu wa mechi ambazo wamecheza na Yanga dhidi ya Simba, mwezi Februari na siku ya Jumamosi wapinzani wao ndiyo wamekuwa vinara.
Rekodi za misimu mitano nyuma zinaonyesha wazi kwamba timu hizo kila zinapokutana kwenye mechi ambayo inachezwa siku ya Jumamosi basi wamekuwa na upepo wa hali ya juu.
Rekodi ambazo Spoti Xtra, limezidaka ni za kuanzia msimu wa 2014/15, ambapo klabu hizo mbili zimekutana mara sita huku wakienda sare mara nne na Yanga kuibuka kidedea mara mbili. Hii ni kwa mechi za watani hao zilizochezwa kwa siku ya Jumamosi tu.
Lakini pia kwa mechi ambazo wamecheza ndani ya mwezi Februari zinaonyesha wazi kuwa Yanga ndiyo wafalme baada ya kucheza mechi sita na kushinda mechi tatu, mbili wakienda sare huku Simba wakishinda moja.
Mechi ambazo Yanga wameshinda ndani ya mwezi Februari ni zile za Februari 26, 1994 Yanga wakishinda kwa mabao 2-0, yaliyofungwa na Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ na James Tungaraza ‘Boli Zozo’ kisha Februari 25, 1996
Mechi nyingine ambazo walishinda Yanga ndani ya mwezi huu ni Februari 20, 2016 ambapo Yanga walishinda kwa mabao 2-0, mabao yake yakifungwa na Donald Ngoma sambamba na Amissi Tambwe. Mechi za Februari 10, 1983 na Februari 21, 1998 walitoka sare huku Simba wakishinda mechi moja tu ya Februari 26, 2017.
Timu hizo zimekutana mara 10 kwenye kwenye mechi za misimu mitano nyuma, huku Yanga wakishinda mechi mbili na mechi tano wakienda sare na Simba wakishinda tatu lakini wao wameshinda Jumapili.
Yanga walishinda Jumamosi, Septemba 26, 2015 mabao 2-0 kisha Februari 20, 2016 mabao 2-0, Simba wao wameshinda Machi 8, 2015 wakashinda Februari 26, 2017 kisha Aprili 29, 2018. Siku zote hizi ni Jumapili.
Ndani ya mwezi Februari Yanga wamevuna pointi tisa wakati Simba wakiambulia pointi moja.
Yanga wamevuna mabao nane wakati Simba wakipata mabao matatu tu.
Jee ni timu gani kati ya hizo mbili iliyofunga mweziwe idadi kubwa zaidi ya magoli?
ReplyDelete