February 11, 2019


Na George Mganga

Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema kwa sasa hawawezi kuzungumzia suala la Kocha Msaidizi kwani wapo kwenye lengo moja la kuhakikisha wanafanikisha ushindi dhidi ya Al Ahly.

Simba itakuwa inacheza na Al Ahly Februari 12 2019 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wa hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kutokana na kukabiliwa na kibarua hicho, Manara ameeleza kuwa nguvu na akili zao kwa sasa zipo kwenye mtanange huo wenye uzito wa aina yao kwao.

Kauli ya Manara imekuja kufuatia kuwepo kwa tetesi kuwa imefanikisha kumsajili Kocha Denis Kitambi aliyewahi kuifundisha Ndanda FC ili kuja kushika nafasi ya usaidizi kwa Mbeligiji, Patrick Aussems.

Manara ameshinda kueleza chochote juu ya Kitambi kwakuwa wanajiandaa na mechi dhidi ya Al Ahly wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi yao kwa mabao 5-0 jijini Alexandria huko Misri.

"Kwa sasa siwezi kuzungumzia lolote juu ya Kocha Msaidizi, tupo kwenye lengo la kuakikisha tunapata matokeo mazuri dhidi ya Al Ahly, mengine yatafuata baadaye" alisema.

1 COMMENTS:

  1. Ni ujinga mtupu kwani kocha msaidizi ni muhimu kuliko hizo blah blah. Kocha msaidizi ni moja ya maamdilizi muhimu kabisa ya mechi inayokuja aijui viongozi wa Simba wanafikiria nini?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic