February 8, 2019


Chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeandika barua kwenda kwa Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA), Infantino kumshitaki Rais wa mpira wa miguu wa Tanzania (TFF) Wallace Karia kwa kumdhalilisha mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chadema, Mh Tundu Lissu.

Katika mkutano mkuu wa TFF wa mwaka 2018 uliofanyika Arusha Karia alinukuliwa akisema kauli inayoeleza kuwa atawashughulikia wakina Tundu Lissu wa soka nchini akimlenga Michael Wambura aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF ambaye amefungiwa maisha kutojihusisha na Soka.




6 COMMENTS:

  1. Litakuwa ni jambo sahihi na linalofaa ili viongozi wote wanaotaka kutumia siasa katika soka iwe fundisho. SOKA NI KIUNGANISHI KWA WATU, SOKA SIO ENEO LA KUENEZA CHUKI NA KASHFA ZA KISIASA.

    ReplyDelete
  2. Sijapenda lugha aliyotumia katika mazingira ya wapenda soka kama TFF ni tawi la ccm tujue. Apelekwe FIFA na pia achunguzwe kwenye upigwaji wa risasi wa Tindu Lissu.

    ReplyDelete
  3. Nashsngaa kwanini Karia aliomba radhi kwa kuzungumza ukweli.Kuna mtanzania gani asiejua yakuwa Tundu Lisu ni mtu wa hovyo katika taifa hili.Hivyo kusema Tundu Lisu ni wa hovyo kuna kosa gani. Yuko wapi Tundu Lisu hivi sasa? Marekani. Shughuli gani iliyompeleka Tundu Lisu Marekani? Ni kwenda kupiga kampeni ya nguvu kahakikisha Tanzania inasusiwa na mataifa ya nje hasa mataifa yenye ushawishi mkubwa duniani. Lakini utaona lengo na hamu yake kubwa Tundu Lisu ni kuingiza Tanzania kwenye mgogoro mkkubwa wa kisiasa na kiuchumi na mataifa ya Magharibi pamoja na kuhakikisha shughuli zote za maendeleo zinazoendelezwa na serikali ya sasa zinakwama. Tundu Lisu kwa Mtanzania mwenye akili timamu sio mtu wa kumchukulia poa hata kidogo ni adui wa dhahiri wa nchi hii sio wa kujificha. Sasa wacha mabumbula waendelee kumsapoti na kumsheherekea. Kumsheherekea mtu anaeifanya jitihada ya kuitia moto nyumba mnayolala mkiwa bado mmo ndani ya nyumba hiyo hapo ndipo utaona kwa kiasi gani watanzania tulivyo watu wa hovyo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. tundu lisu ni mkombozi wa taifa huru katiba ya nchii inavunjwa mmekaa kimya anacho kisema tundu lisu ni ukweli mtupu yupo wapi beni sanane,yupo wapi mawazo uchunguzi umeishia wapi alie mpiga tundulisu risasi ajulikani mpaka leo uwoni ni aibu kwa vyommbo vyetu vya ulinzi mpaka leo kimyaaa

      Delete
  4. Tundu Lisu mkombozi wa taifa huru? Kwanza angeanza kuikomboa chadema iwe huru kutoka kwenye utawala wa Mbowe na familia yake.

    ReplyDelete
  5. Mhu! Sasa hii ni siasa, na wala sio michezo jamani!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic