February 8, 2019


KAMATI ya Tuzo ya Ligi Kuu Bara imemteua kocha mkuu wa KMC, Ettiene Ndayiragije kuwa kocha bora wa mwezi Januari.

Ndiragije amewashinda makocha aliofika nao hatua ya fainali ambao ni Kocha Mkuu wa Alliance, Malale Hamsini na Kocha Mkuu wa Biashara United Amri Said.

Ndiragije alifanikiwa kuiongoza timu yake katika michezo minne kushinda yote na kukusanya pointi 12 ambazo ziliifanya ipande nafasi kwenye msimamo kutoka nafasi ya 10 mpaka nafasi ya tatu.

Pia Kamati imemteua mshambuliaji wa timu ya Alliance, Dickson Ambudo kuwa mchezaji bora wa mwezi Januari.

Ambundo amewashinda wenzake wawili ambao ni mlinda mlango Juma Kaseja wa KMC na mshambuliaji wa Coastal Union Ayoub Lyanga.

Ambundo katika michezo mitano ambayo Alliance walicheza mwezi Januari aliisaidia timu yake kupata pointi 11 baada ya kushinda michezo mitatu na sare michezo miwili na kujikusanyia pointi 11 huku yeye akifunga mabao matatu.

2 COMMENTS:

  1. Hivi kushinda mechi tatu nakutoa sare unakuwa napoint ngapi?au Sikh hizi ukitoa sare unapewa points 2?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Brother, wewe ndiye ambaye hujaelewa. Wameshinda michezo mitatu (Points 9), Sare michezo miwili (Points 2). Hivyo, Points 9 + 2 = 11. Wapo sahihi, soma vizuri Paragraph ya mwisho.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic