February 12, 2019



DARUESH Saliboko wa Lipuli FC jana aliwalazimisha Azam FC kusubiri mpaka dakika ya 80 kufunga bao la kusawazisha baada ya kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao moja lililofungwa dakika ya 45.


Wakiwa uwanja wa nyumbani Samora, Lipuli ya Matola ilishindwa kulinda bao lao.

Salum Abubakari alitumia vema nafasi aliyopata akiwa ndani ya 18 na kuachia shuti kali mbele ya walinzi wa Lipuli lillilomshinda mlinda mlango wa Lipuli.

Matokeo hayo yanaifanya Azam FC kufikisha pointi 49 wakiwa nafasi ya pili huku Lipuli ikiwa na pointi 37 nafasi ya tatu wanaishusha Simba na kutinga tatu bora.

1 COMMENTS:

  1. Na baada ya kusema kuwa Lipuli kachukua nafasi ya tatu na kuiteremsha Simba kuwa nafasi ya nne, ilibidi urache idadi ya mechi iliyocheza Simba na zile za Lipuli

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic