SALUM Aiyee wa Mwadui FC jana aliibeba timu yake kwa kuisaidia kubakiza pointi tatu nyumbani kwenye Uwanja wa Mwadui Complex dhidi ya Mtibwa Sugar.
Bao lake moja la ushindi lilifungwa dakika ya 75 kipindi cha pili baada ya dakika 45 za kwanza kumalizika kwa timu zote kushindwa kuona lango la mpinzani.
Ushindi huo unamfanya Aiyee azidi kuwapoteza washambuliaji wa Simba, Meddie Kagere mwenye mabao nane na Emmnuel Okwi mwenye mabao saba.
Matokeo hayo yanaifanya Mwadui kuwa nafasi ya 16 baada ya kucheza michezo 26 wakiwa na pointi 27 huku Mtibwa wakishuka kutoka nafasi ya 10 mpaka ya 11 wakiwa na pointi 29.
Pia Tanzania Prisons licha ya kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Stand United wamebaki nafasi ya 17 wakiongeza pointi tatu na kufikia 26 mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine.
Suluhu ya African Lyon dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru iliwatoa nafasi ya 20 na kuwapandisha mpaka nafasi ya 19 wakiwa na pointi 21 huku Ruvu Shooting wakipanda mpaka nafasi ya 10 kutoka nafasi ya 13 baada ya kufikisha pointi 30.
Ndanda walishinda mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar wanabaki nafasi ya 18 wakiwa na pointi 26 baada ya kucheza michezo 24 huku Kagera Sugar wakishuka kutoka nafasi ya 14 mpaka ya 15 wakiwa na pointi 28.

0 COMMENTS:
Post a Comment