YANGA KUUKOSA UBINGWA WA LIGI KUU BARA KWA MISIMU 10 IJAYO
Wakati kikosi cha Simba kikiendelea kula viporo vyake, uongozi wa timu hiyo umesema malengo yake ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa misimu 10 ijayo mfululizo.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameeleza kwa kikosi walichonacho hivi sasa kinawapa jeuri hiyo.
Manara ameeleza kuwa wanataka kuifikia na ikiwezekana kuizidi mataji Yanga ambayo imetwaa mara 27 huku Simba wakiwa wamechukua mara 18 tu.
Simba wikiendi hii itakuwa na kibarua kingine cha ligi mjini Shinyanga na kuelekea mechi hiyo Manara amesema wamejipanga vizuri.
Tayari kikosi kipo njiani na Kocha Mkuu, Mbelgiji Patrick Aussems amesema wanaenda kupigania alama tatu muhimu kujiwekea mazingira mazuri ya kuchukua ubingwa.
Yes we can
ReplyDeleteInatakiwa transparent and accountability katika bodi ya usajili uzingatiwe,kama club imeamua kusajili mchezaji basi ni bora vigezo na sifa viwekwe wazi kabla yakufanya usajili,me naona hilo linaweza likasaidia timu kufanya vizuri,mchezaji aanikwe wazi kuanzia alikoanzia kucheza soka mafanikio yake binafsi katika kuchukua mataji,mafanikio ya kitimu katka kuisaidia kupata matokeo bora,na je ana uwezo gani kwa sasa pia thamani kulingana na uwezo wake,kama tumedhamiria jamani bora ifanyike haswa kwasababu inawezekana tena kwa kiwango cha juu kabisa,na hii sio kwa simba tu hata azam,yanga na clubs zingine za kibongo inawezekana, shime jamani.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteHukutaja inakwenda kupambana na yimu gani
ReplyDeleteAya ya pili kutoka chini......."Simba wikiendi hii itakuwa na kibarua kingine cha ligi mjini Shinyanga na kuelekea mechi hiyo Manara amesema wamejipanga vizuri".
Delete