February 7, 2019


MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere anawanyanyua mashabiki wa Simba kwa kufunga bao la kwanza kwa kichwa katika mchezo wa leo dhidi ya Mwadui, pasi ya Clatous Chama baada ya Haruna Niyonzima kupiga kona fupi dakika ya 21.

Mzamiru Yassin alifanya hivyo tena dakika ya 26 akimalizia pasi aliyotengewa kwa kifua na nahodha John Bocco,dakika ya 29, Niyonzima alipipiga pasi iliyomfikia Bocco alicheka na nyavu kwa kichwa na kufanya idadi ya mabao kufika 3-0.

Kwa sasa mpira ni kipindi cha pili, mashabiki wamejitokeza kwa wingi kuona namna msisimko wa Ligi Kuu Bara unavyoendelea.

Ushindani ni mkubwa huku kipindi cha kwanza Mwadui walikuwa wakishambulia kwa kushtukiza na kujilinda na Simba walikuwa wakishambulia mara kwa mara.

Aussems wa Simba alifanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kumtoa Kagere nafasi yake ikachukuliwa na Adam Salamba, Mzamiru Yasin aliumia nafasi yake ikachukuliwa na Jonas Mkude na Chama alitoka nafasi yake ikachukuliwa na Emanuel Okwi.

Mpaka dakika tisini zinakamilika mchezo wa leo Simba wanaondoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 3-0.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic