February 15, 2019



PATRICK Aussems, kocha mkuu wa Simba amesema kinachompa nguvu ya kusonga mbele ni ushindi wa kikosi chake mbele ya waarabu alioupata Jumanne ya wiki hii kwenye Uwanja wa Mkapa.

Simba kesho watakuwa wageni kwa Yanga ikiwa ni mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Bara majira ya saa 10:00 jioni.
Aussems amesema atatumia mbinu kama zile alizotumia kumchinja mwarabu kupata matokeo mbele ya vinara wa ligi Yanga.

"Tumeshinda mchezo wetu mgumu wa Ligi ya Mabingwa, kinachofuata ni ushindi mbele ya Yanga, nitatumia mbinu zile nilizotumia kwa Al Ahly kupata matokeo mbele ya wapinzani wangu," amesema Aussems.

Yanga ni namba moja kwenye msimamo wakiwa na pointi 58 baada ya kucheza michezo23 huku wapinzani wao wa karibu Simba wapo namba nne wakiwa na pointi 36 baada ya kucheza michezo 15.

2 COMMENTS:

  1. Kwa mchina bana kwa Mkapa hatukujui

    ReplyDelete
  2. Alianza Azam kupoteza mechi ya kwanza mbele ya Mtibwa, Akafuatia Yanga nae mbele ya Stand United. Akaanza tena Azam kupoteza mechi ya pili mbele ya Prisons hapo jana, na sasa anafuatia tena Yanga kupoteza mechi ya pili mbele ya Simba hapo kesho. Baada ya hapo nina imani wataanza kugoma na wengine kufukuzana ili kuifagilia njia ya Ubingwa wa mara ya pili mfululizo wa Simba. Sisi ni WAGENI WASIO NA ADABU.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic