February 18, 2019



MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere amesema kuwa hana habari na kazi ya kujitamba kwenye mitandao ya kijamii badala yake ataonyesha kazi kubwa uwanjani.

Kagere ameendeleza makali yake Ligi Kuu Bara kwa kufunga mabao mawili kwenye mechi mbili mfululizo akianza ule wa Mwadui FC na mchezo wa watani wa jadi Yanga uwanja wa Taifa kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 71.

"Sina habari na kazi za kwenye mitandao ya kijamii kazi yangu mimi uwanjani, huku ndiko hasira zangu zilipo, yale ambayo yamepita kwangu ni historia nafanya mipango mingine," amesema Kagere.

Kagere anafikisha mabao tisa kwenye msimamo wa wafungaji huku kinara akiwa na Herieter Makambo wa Yanga mwenye mabao 11.

2 COMMENTS:

  1. Ataongeza mengine mwaili katika mechi na Lyon na kuzidi kupachika katika kiporo na zijazo. Kutangulia si kufika

    ReplyDelete
  2. Basi la barafu limeanza kuyeyuka kabla ya kufika kituo cha mwisho. Treni la mwendo kasi tena la chuma linakuja kwa spidi zote. Hilo halina joto wala baridi, lazima lifike mwisho.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic