KOCHA wa Azam FC, Hans Pluijm amesema kuwa kikosi chake kushindwa kupata matokeo ni upepo mbaya tu ambao unapita kwa muda.
Azam FC walianza kupata sare mbele ya Alliance wakiwa nyumbani Chamazi kisha wakalazimisha sare dhidi ya Lipuli FC wakiwa Samora kabla ya kupoteza mbele ya Prisons Uwanja wa Sokoine.
Pluijm amesema kuwa bado kikosi kina nafasi ya kufanya vema kwenye michezo yao inayofuata kikubwa ni sapoti na wachezaji kuendelea kujituma.
"Hakuna tatizo katika matokeo ambayo tunayapata, natambua kwamba hesabu zetu ni kupata matokeo ila ushindani uliopo unafanya haya yatokee, makosa tunayafanyia kazi hivyo baada ya muda kila kitu kitakuwa sawa," amesema Pluijm.
Azam FC wamecheza michezo 23 wakiwa nafasi ya pili na wana pointi 49 huku kinara akwa ni Yanga mwenye pointi 58 baada ya kucheza michezo 24.
Mwenzake Zahera anasingizia TUNGURI ����������
ReplyDeleteHuo ndo utofauti wa Mshirikina na Mtaalamu. Zahera anaamini kila mafanikio yanatokana na ushirikina, lakini Pluigm anaamini kuwa kila mafanikio yanatokana na uwezo wa kujituma na mbinu. Viti vya watu hivyo huko juu, naona wanaanza kuregeza kamba.
ReplyDelete