MKUDE ATAKIWA KUONDOKA SIMBA
Na George Mganga
Mchezaji wa zamani wa Yanga, Simba na Taifa Stars, Bakali Malima, amemtaka kiungo wa Simba, Jonas Mkude kujiengua katika soka la Tanzania ili kwenda kimataifa zaidi.
Kwa mujibu wa Radio One, Malima ambaye aliwahi kung'ara ndani ya timu hizo mbili, ameeleza kuwa ni wakati mwafaka wa Mkude kucheza soka la kimataifa kutokana na uwezo wake uwanjani.
Mchezaji huyo wa zamani ameonesha kushangazwa kwanini Mkude mpaka leo anachezea Simba na ilihali kwa uwezo alionao uwanjani anapaswa kucheza soka la kimataifa.
"Unajua nashangaa mpaka sasa Mkude yupo hapa nchini, muda unaenda na ni wakati wake sasa kucheza soka la kimataifa kwani ana uwezo wa hali ya juu" alisema.
Kauli ya Malima imekuja mara baada ya mchezo wa jana dhidi ya Yanga ambao ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 likipachikwa na Meddie Kagere.
0 COMMENTS:
Post a Comment