BAADA YA KUWA KIMYA TANGU ATUE NCHINI, ZANA ATOA TAMKO LAKE RASMI SIMBA
Beki Zana Coulibally amewashukuru mashabiki wa Simba ambao walionyesha kumuunga mkono wakati akiendelea kurejea katika kiwango chake.
Zana amefanya hivyo mara tu baada ya mechi dhidi ya Yanga na Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Meddy Kagere.
Mara tu baada ya mechi, Zana aliwafuata mashabiki wa Simba na kuwaonyesha ishara ya shukurani na baadaye kusema, walimvumilia na sasa ameanza kupata kiwango chake.
Baada ya kutua nchini, Zana alikuwa gumzo akionekana hana kiwango kizuri kama ambavyo wengi walitarajia.
Hata hivyo ilielezwa hakuwa katika kiwango kizuri kwa kuwa hakuwa amecheza kwa muda mrefu
Ni imani kubwa sana kuwa, beki huyu atakuwa tishio kubwa sana kwa Afrika nzima. Simba wanatakiwa kumtumia vizuri. Kwa uchezaji wake unaovutia, na wenye maarifa, amekuwa ni mzuri sana katika kucheza mpira na kumzuia adui bila kusababisha faulo yoyote. Ni mara chache sana m,wanzoni amekuwa anakosa umakini, lakini kwa kadri alivyopewa mechi mfululizo, ameonekana kuendelea kujiamini na kupunguza makosa aliyoyasababisha mechi iliyopita. Zaidi namuomba aendelee kujiamini. NAMKUBALI.
ReplyDelete