February 8, 2019


UONGOZI wa Simba umewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi katika mchezo wao wa marudiano dhidi ya Al Ahly ambao ni wa Ligi ya Mabingwa utakaochezwa Februari 12, Uwanja wa Taifa.

Simba inakumbukumbu ya kupoteza michezo yake miwili ya ugenini katika hatua ya makundi hivyo deni lao kubwa ni kufanikiwa kushinda katika michezo yake mitatu iliyobaki.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Simba Sports Club, Mohammed Dewji 'Mo' amesema malengo makubwa ya klabu ni kuona inafanikiwa kupata matokeo chanya.

"WanaSimba na Watanzania kama tutajitokeza kwa wingi siku ya jumanne nina imani tutawafunga Al Ahly na tukiwafunga tutakuwa na nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Shabaha yetu ilikuwa kufika kwenye makundi na tumefanikiwa na shabaha yetu nyingine ni kutetea kombe la Ligi Kuu ili tuendelee kushiriki mashindano haya," alisema.

Mwenyekiti wa Simba, Sued Mkwabi amesema kwamba "Simba ikifanya vizuri faida ni kwa nchi yetu kuweza kupata mwakilishi zaidi ya mmoja kwenye mashindano yajayo, muhimu Wanasimba na wasio Wanasimba wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yetu ambayo ndio inawakilisha nchi yetu kwenye mashindano ya kimataifa,".

Simba wapo kundi D kwenye hatua ya makundi ambapo kinara ni Al Ahly akiwa na pointi nne akifuatia na AS Vita ambaye ana pointi tatu huku Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi tatu na JS Saoura wanashika nafasi ya nne wakiwa na pointi mbili.

Wapinzani wao Al Ahly wanatarajiwa kutia timu alfajiri ya kesho tayari kwa mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa.

1 COMMENTS:

  1. Lakini Mo Dewji na Simba kwa ujumla haya malengo ingawa ni mazuri kuyafikia ni lazima Ligi ya Tanzania ikue na wanaoiendesha waiendeshe kwa weledi mfumo wetu wa ligi, ratiba za mashindano, ubora wa timu za ligi, waamuzi vyote vinachangia....ili Simba ifanikiwe lazima timu za ligi ziwe bora kuipa ushindani....Yanga mbovu mtibwa mbovu ndanda mbovu haitoisaidia Simba katika pale inapopataka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic