Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali amesema amesikitishwa na taarifa zinazosambazwa mtandaoni kwamba anapinga suala la mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji kuwa anataka hati za majengo ya Simba.
Kuna taarifa imekuwa ikisambazwa mitandaoni na inaelezwa kuwa ili Dewji atoe fedha hizo za uwekezaji anataka apewe hati ya majengo ya Simba.
"Kwa kweli nimeshangazwa sana na hali hii, naona kama kuna watu wanataka kuichanganya Simba au kunigombanisha na Simba tu," alisema Mzee Dalali.
"Vipi mimi nipinge wakati nimesaidiana na watu kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa, hawa watu ni watu wa aina gani na wanataka nini haa sielewi wanataka nini kwangu.
"Hawa wanaosambaza ni watu ambao wanaotaka nionekane ni mtu mbaya. Lakini hawatafanikiwa na ukweli Simba iachwe kipindi hiki kwa kuwa ina mechi ngumu za Ligi ya Mabingwa, wanajiweka sawa kugombea ubingwa," alisisitiza.
"Sipendi kutumika au kufanywa sehemu ya kuiyumbisha Simba, nikiwa na hoja yangu ntaweka wazi, watu wasinilishe maneno."
Hakuna mwanasimba anaesambaza habari hizo za uchonganishi ni wapumbavu kutoka mtaa wa jirani.Ni habari zianazosambazwa na watu wa Yanga baada ya kufulia kiuongozi katika timu yao sasa wanaishia kuiwangia Simba usiku na mchana ili iingie kwenye matatizo lakini kwa Simba hii ya sasa mtashindwa wenyewe na fitina zenu.
ReplyDeleteSimba sasa ni taasisi. Fitina za ghahwa pelekeni mtaa wa pili.
ReplyDeleteLakini Mo Dewji na Simba kwa ujumla haya malengo ingawa ni mazuri kuyafikia ni lazima Ligi ya Tanzania ikue na wanaoiendesha waiendeshe kwa weledi mfumo wetu wa ligi, ratiba za mashindano, ubora wa timu za ligi, waamuzi vyote vinachangia....ili Simba ifanikiwe lazima timu za ligi ziwe bora kuipa ushindani....Yanga mbovu mtibwa mbovu ndanda mbovu haitoisaidia Simba katika pale inapopataka
ReplyDelete