MSUVA AIBUKIA SIMBA
WINGA wa Klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco, Simon Msuva, amemwambia kiungo mpya wa ENPPI ya Misri, Shiza Kichuya kuwa anatakiwa kupambana kwelikweli na kutokubali tena kurudi kucheza soka Tanzania.
Hivi karibuni Kichuya alikamilisha dili la kujiunga na Klabu ya Pharco ya Misri ambayo yenyewe imemtoa kwa mkopo ndani ya Klabu ya ENPPI ambayo ipo ligi kuu.
Msuva ambaye ana mwaka na nusu ndani ya Klabu ya Difaa, ameliambia Championi Jumatano, kuwa anafurahia kuona namba ya wachezaji wanatoka nje ya Tanzania inaongezeka huku akiwataka wachezaji hao kuhakikisha wanapambana vya kutosha kwa ajili tu ya kutorudi tena nyumbani.
“Kwa upande wa wachezaji ambao sasa hivi wanazidi kutoka nje ni kitu kizuri na cha kumshukuru Mungu kwani tunapanua wigo wa timu ya taifa.
“Ukiangalia timu ya taifa kwa miaka ya nyuma ilikuwa inashindwa kufanya vizuri kwa sababu wachezaji wengi walikuwa wa ndani, ni kitu kizuri tunapoongezeka wachezaji tunaocheza nje.
“Nawapongeza wanaoendelea kutoka huko nyumbani, kikubwa ninawashauri ndiyo wameanza safari, hivyo hawatakiwi kukata tamaa.
Japo nina mwaka na nusu huku Morocco, lakini nina uzoefu japo siyo mkubwa wa kuweza kumshauri mtu tofauti ya soka la ndani na nje,” alisema Msuva
kichwa cha habari na kilichozungumzwa ndani ni tofauti
ReplyDeleteWaandishi hawa kwanini usiwe mbunifu kuandika heading mzuri inayoendana na yaliyomo?
ReplyDelete