BEKI SIMBA ACHUNGUZWA FIFA
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa), limeanza uchunguzi makini dhidi ya beki wa zamani wa Simba, George Uwino ambaye inasemekana alilipwa mamilioni ya shilingi ili kuuza mechi za timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars.
Katika ripoti ya awali yenye kurasa 10 iliyoonwa na Gazeti la Nation, Fifa imeamua kumuanzishia kesi Owino kwa kukiuka maadili nyeti ya shirikisho hilo la kimataifa kati ya Juni 2009 na 2011.
Kwa mujibu wa ripoti ya Fifa iliyotolewa Septemba 2018, Owino, 37, kupitia meseji 177 kati yake na mpanga matokeo mkubwa wa kimataifa, Wilson Raj Perumal, ilibainika kuwa nyota huyo na jamaa huyo walikubaliana auze mechi za kimataifa zinazoihusisha Kenya.
Fifa imesema Owino, 37, alikubali akiwa pamoja na baadhi ya wachezaji wa Harambee Stars wacheze sawasawa na maelekezo ya Perumal.
Taarifa zaidi za mechi 14 zilizotajwa kama uthibitisho, bado zimeshikiliwa na Idara ya Maadili ya Fifa, ambayo iliwasiliana na Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) Agosti 10, 2018 ikihitaji mikataba ya Owino.
Perumal aliwahi kufungwa nchini Finland na Hungary kwa makosa ya kupanga matokeo. Owino aliichezea Simba kwa msimu mmoja wa 2007-08. Pia aliwahi kuichezea Yanga mwaka 2009.
Hata Simba wachunguzwe kunako hizi mechi mbili za 5+5? Zinatia mashaka sana kwa jinsi wachezaji walivyopooza uwanjani kama vile walikuwa wakisumbuliwa na matumbo ya kuharisha. Kwa hivi vigogo viwili As vita na Ahly sijui nani anamzidi mwenzie kwa fitina na wana uwezo wa pesa so anything is possible tusichukulie kirahisirahisi tu kuwa Simba imefungwa kwa kuzidiwa mpira. Hata kuuza mikakati ya mechi kwa timu pizani kabla ya mechi ni upangaji wa matokeo pia. Ndio maana utawashngaa viongozi wa Simba kuwaachia wachezaji wao kuwa free kwenye hizi mechi zao zote walizocheza na aiza Ahly au As vita wakati kama ingewezekana ni kuwaweka kambini wachezaji wao wiki mbili kabla ya mechi nakuwa karibu zaidi na Simu wachezaji wao wanawasiana na nani kwani kwa hali ilivyo anything is possible.
ReplyDeleteMmh Kuna haha gani kuandika kichwa Cha habari kuwa 'beki wa Simba anachunguzwa' wakati so mchezaji was Simba kwa Sasa?
ReplyDelete