February 16, 2019




LEO jumamosi ya Februari 16 Uwanja wa Taifa kutakuwa na mchezo wa watani wa Jadi, Yanga na Simba ambao ushindani wake ni mkubwa.

Simba wao watakuwa kwenye kazi mpya kumtafuta atakayeamua matokeo kutokana na nyota wao Shiza Kichuya kupata timu ya kucheza msimu huu nchini Misri ya ENPPI inayoshiriki Ligi Kuu.

Kichuya alipokuwa na Simba alikuwa na uwezo wa kuamua matokeo wakati Simba ikiwa imefungwa na wapinzani hao ama wakati wakiwa sare.

Rekodi zinaonyesha kuwa Kichuya amekuwa na uwezo wa kuamua matokeo kwenye mechi za watani wa jadi alianza mwaka 2015/16 Simba walipokuwa nyuma kwa bao moja lililofungwa dakika ya 26 na Amiss Tambwe.

Kichuya alisawazisha kwa kufunga bao la kona goli dakika ya 87 hali iliyowafanya wagawane pointi mojamoja Uwanja wa Taifa.

 Msimu wa mwaka 2016/17  bao la Kichuya liliamua matokeo baada ya kufunga dakika ya 81 kwenye ushindi wa mabao 2-1.

Yanga walianza kufunga dakika ya tano kwa mkwaju wa penalti iliyowekwa kimiani na Simon Msuva ambaye kwa sasa yupo Al Jadida ndipo dakika ya 66 Laudit Mavugo alisawazisha na Kichuya alifunga bao la ushindi dakika ya 81.

Pia Kichuya alitoa pasi ya bao la ushindi msimu wa 2017/18 Uwanja wa Taifa baada ya kupiga mpira wa faulo uliowekwa kimiani kwa kichwa cha Erasto Nyoni baada ya Kelvini Yondani kumchezea rafu beki kiraka Shomari Kapombe dakika ya 34.

Mtihani mpya kwa Simba ni kutokana na kuwakosa Shomari Kapombe na Erasto Nyoni ambao wanasumbuliwa na majeruhi licha ya Nyoni kuanza mazoezi ila bado hajawa fiti kuanza mechi za ushindani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic