February 16, 2019



Mzunguko wa pili Yanga inatakiwa kucheza mechi nyingi zaidi ugenini, tayari kocha wa kikosi hicho, Mwinyi Zahera anaona kuna kitu hakipo sawa kwa TFF na kinapaswa kufanyiwa kazi.

Baada ya wikiendi iliyopita Yanga kutoka na pointi tatu Tanga mbele ya JKT Tanzania vigongo vyake vya kukamilisha mwezi huu vipo namna hii:-

Leo, Februari16, itamenyana na Simba jijini Dar es Salaam, kisha Februari 20 itakuwa Mwanza kumenyana na Mbao.

 Baada ya hapo, itasafiri mpaka Lindi kucheza mechi ya Kombe la FA dhidi ya wenyeji wao, Namungo FC. Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa kati ya Februari 22 na 25, mwaka huu.

Yanga ni kinara wa Ligi Kuu Bara, amecheza michezo 23akiwa amejikusanyia pointi 58, amepoteza mchezo mmoja na kutoa sare michezo minne

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic