February 6, 2019


UONGOZI wa Mwadui FC umefunguka kuwa umejipanga kuhakikisha unaibuka na ushindi na kulipa kisasi kwa Simba baada ya kupoteza mchezo wao wakiwa nyumbani walipokutana mwaka jana.

Katika mzunguko wa kwanza Mwadui FC iliambulia kipigo cha mabao 3-1 katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Kesho Alhamisi timu hizo zitavaana katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam katika mwendelezo wa ligi.

 Katibu wa timu hiyo, Ramadhani Kilao alisema kocha wao Ally Bizimungu anendelea kufanya maandalizi kuona anaondoka na ushindi mbele Simba.

“Kocha wetu amefanya maandalizi ya kutosha na kama unavyofahamu hiki ni kipindi cha lala salama sisi kama timu tunahitaji kupata pointi tatu mbele ya Simba kulipa kisasi cha kipigo ambacho tulipata nyumbani.

“Tunafahamu kuwa nao wamejiandaa na wametoka kujeruhiwa huko kwa kufungwa, tutakuwa makini na tutapambana na kuondoka na matokeo mbele yao hili kuwa katika nafasi nzuri,”alisema Kilao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic