February 6, 2019


OFISA Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Simba, Crescentius Magori, ametamba kuwa matokeo mabaya waliyoyapata wapinzani wao AS Vita na JS Saoura yamewapa matumaini ya wao kufuzu katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kauli hiyo aliitoa juzi baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam walipotokea Misri kucheza na Al Ahly katika mchezo wa hatua ya makundi ya michuano hiyo na Simba kufungwa mabao 5-0.

Mchezo wa AS Vita na JS Saoura ulimalizika kwa matokeo ya sare ya kufungana mabao 2-2 ambayo Simba kama ikifanikiwa kupata ushindi kwenye michezo yake miwili ya nyumbani itakuwa na matumaini ya kufuzu.

Akizungumza na Championi Jumatano, Magori alisema matokeo hayo ya sare kati ya AS Vita na Saoura yamewarudisha mchezoni kutokana na uchache wa pointi walizoachana katika kundi lao D.

“Mashabiki wa Simba wasikatishwe tamaa ya kufuzu hatua inayofuata ya michuano hii, kikubwa wanachotakiwa ni kuungana kwa pamoja na kuweka mikakati thabiti ya ushindi ya michezo yote miwili tutakayocheza hapa nyumbani.

“Ukiangalia kwenye kundi letu, Al Ahly pekee ndiyo yenye nafasi ya kufuzu hadi hivi sasa ambayo imejikusanyia pointi saba ikifuatiwa na AS Vita yenye nne tukifuatiwa na sisi wenye tatu.

“Hivyo, utaona ni jinsi gani bado tuna nafasi ya kufuzu hatua inayofuata, hivyo sisi Simba na AS Vita tunagombania nafasi moja ya kufuzu na yeyote ana nafasi ya kufuzu kwa atayepata matokeo mazuri katika michezo yake ijayo,” alisema Magori.

1 COMMENTS:

  1. Habari za kwamba kuna wachezaji wa Kenya walihusika kuuza mechi kwa kushirikiana na cartel matata na dalali maarufu wa gizani wa kurubuni wachezaji au hata viongozi wa timu kuuza mechi msingapori pameru ni za kutia kichefuchefu. Inamaana mchezo wa kuuza mechi za kimataifa upo na unafanyika kwa siri kubwa. Kwa kiasi fulani kuamini kuwa timu zetu zinafungwa kutokana na kuzidiwa kwa ukubwa na baadhi ya timu vigogo vya Africa bila ya kufanya ucbunguzi na kujiridhidha juu ya matokeo halisi nadhani tunaweza tukajikuta tukiwapa kazi rahisi wapiga dili hao. Sio siri licha ya Simba kuzidiwa viwango na As vita na Elahly lakini yale matokeo yanatia mashaka na nadhani takukuru ipo haja ya kuchunguza matokeo ya mechi mbili za Simba za club bingwa. Kitu kimoja cha ajabu kuna wadau wa mpira hapa nchini ambao wana lazimisha kuwaaminisha watanzania kuwa timu zetu lazima zifungwe tu na timu za nje iwe, isiwe kwa kisingizio cha viwango, kwanini? Wana uhakika gani?
    Hawa watu wasijekuwa ni mawakala wa mashetani wanajificha chini ya sababu za kiwango kidogo cha timu zetu kumbe wapiga dili. Sisemi kwamba timu zetu haziwezi kufungwa ila hizi taarifa za achezaji wa Kenya katika kuuza mechi inaonekana kabisa yakwamba kama kuna ujasiri wa kuuza mechi za timu ya taifa? Kwa klabu itakuwaje?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic