February 9, 2019


MAISHA ya winga kipenzi cha mashabiki wa Simba, Shiza Kichuya yanakwenda kubadilika kwa kiasi kikubwa. 

Alianza mwaka akiumiza kichwa kujua hatma yake ndani ya kikosi cha kwanza cha Simba lakini ghafla dodo likamwangukia na amekuwa wa kimataifa sasa. Kichuya kama hakuwa kazini Simba alikuwa akipatikana Morogoro.

Lakini kuanzia sasa Kichuya atakuwa anapatikana Jijini Cairo, Misri kwa muda akiichezea ENPPI FC kwa mkopo kabla ya kurejea kwenye klabu yake ya Pharco FC. 

Hii Pharco imeasisiwa miaka 10 iliyopita na sasa inashiriki Ligi Daraja la Pili, maskani yao yakiwa Jijini SHIZA KICHUYA wa Kimataifa Alexandria ambao ndio mji wa pili kwa ukubwa wa kibiashara nchini Misri.

Kichuya amekuwa wa kimataifa sasa. Pharco imemnunua Simba kwa Sh196Milioni na kila kitu wameshamalizana. PHARCO FC Ni miongoni mwa timu maarufu kwenye Ligi Daraja la pili ambayo inajijenga ili kupanda daraja.

Imewekeza kwa Kichuya na kumtoa kwa mkopo ili akaimarike zaidi arudi kuwa mkombozi wao. Mpaka sasa wameshacheza mechi 34, wameshinda 18 na sare 11 lakini michezo mitano wamepoteza. Wana pointi 65 wakishikilia nafasi ya nne kwenye msimamo wenye timu 18.

ENPPI FC Ni timu ya matajiri wa Petroli. Imeshiriki mara kadhaa kwenye michuano ya kimataifa ikafanya vizuri hadi kwenye hatua za makundi.

Ni miongoni mwa klabu kubwa za Misri na wako vizuri kiuchumi. Ina wachezaji kutoka DR Congo, Nigeria, Ivory Coast na sasa anaongezeka Mtanzania aliyezaliwa Morogoro. Kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Misri msimu huu wako nafasi ya 14 wakiwa na pointi 21 katika michezo 20.

Msimu huu hawako vizuri wameshinda mechi nne tu na kutoa sare tisa na kupoteza michezo saba. Kocha Ali Maher anaamini ujio wa Kichuya na kile alichokiona kwenye video zake atabadilisha kitu katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo. 

Ligi Kuu ya Misri ina miamba mikubwa kama Al Ahly, Zamalek na Ismailia ambazo zote zimewahi kuja Bongo kucheza na Simba na Yanga.

1 COMMENTS:

  1. Simba ndio mpango mzima muache Ajibu ajicheleweshe kilicho kwenye brand ni rahisi kuuzika.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic