SIMBA YATOA TAMKO RASMI JUU YA KIBARUA CHA HAJI MANARA
Na George Mganga
Baada ya kuwepo kwa tetesi zinazosema kuwa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kuwa anaweza akaondolewa katika nafasi yake, Mwenyekiti wa klabu, Swed Nkwabi, amekanusha suala hilo.
Kumekuwa na maandiko tofauti-tofauti mitandaoni yakisema kuwa Manara anaweza kuondoshwa kwenye nafasi hiyo lakini Nkwabi ameibuka na kusema hakuna ukweli wowote.
Kwa mujibu wa Radio EFM, Kwambi ameeleza kuwa bado wanamtambua Manara kama Msemaji wa klabu na ataendelea kutumikia wadhifa wake kwa kuwa amekuwa na mchango mkubwa.
Mwenyekiti huyo amesema yawezekana labda kumekuwa na mipango ya kuivuruga klabu haswa kipindi hiki timu yake ikiwa katika maandalizi ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.
"Hapana, Haji Manara bado ni msemaji wa Simba, ukiangalia hata jana kupitia Instagram yake aliandika kuhusiana na masuala mbalimbali ya klabu pamoja na kwenye ukurasa rasmi wa timu, si kweli kuwa ataondoshwa" alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment