February 15, 2019


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema haina mamlaka ya kumfutia kesi wala kumpa dhamana Michael Wambura baada ya Wakili wake Majura kuiomba imfutie mashitaka mteja wake kwa madai kwamba mashtaka  hayo sio ya uhujumu uchumi.

Wambura anakabiliwa na mashtaka 17 ambayo anadaiwa kuyatenda  katika ofisi za TFF, kati ya Julai mwaka 2004 na mwaka 2015.

Inadaiwa kuwa Julai 7, mwaka 2004, Wambura alighushi barua akaiwasilisha TFF akijifanya barua hiyo imeandikwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jek System Limited ikidai malipo ya mkopo wa Dola za Marekani 30,000  zilizokopwa na TFF pamoja na riba.

Wambura anadaiwa alijipatia fedha hizo kwa nyakati tofauti na anashtakiwa kwa mashtaka mawili ya kutakatisha fedha ambapo, kati ya Agosti 15 na Oktoba 24 alitakatisha Sh 25,050,000 na 75,945,024 huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la kughushi. 

Kesi imeahirishwa hadi February 28 mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic