February 16, 2019


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Simba umemtangaza rasmi Denis Kitambi kuwa Kocha Msaidizi wa timu yao.

Kitambi ambaye alikuwa kwenye tetesi za kuchukua nafasi ya Masoud Djuma aliyeondoka baada ya kukosa maelewano na Kocha Mkuu, Patrick Aussems, sasa amethibitishwa rasmi kuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu hiyo.

Aussems sasa anaungana na Kitambi baada ya kuwa peke yake kwenye benchi hilo kwa miezi kadhaa tangu kuondoka kwa Djuma aliyepo kwao Burundi.


Kitambi atakuwa sehemu ya mchezo wa leo katika Ligi Kuu bara dhidi ya Yanga utakaoanza majira ya saa 10 jioni.

Simba inaenda ikiwa mgeni wa mchezo huo ambao unasubiriwa kwa hamu na wadau pamoja na mashabiki wa soka nchini Tanzania.

1 COMMENTS:

  1. Safi sana tunahitaji wazawa waelewa kama Denisi katambi kuwa chini ya makocha wenye uzoefu kama Ausems ili waje kuwa msaada kwa Taifa baadae.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic