February 15, 2019


KOCHA wa kikosi cha Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa kinachoziponza timu nyingi kupoteza pointi uwanjani ni pamoja na ubovu wa viwanja.

Matola amesema kuna umuhimu wa wahusika kuweka mikakati maalumu hasa kwa ajili ya msimu ujao kuona namna gani timu zinaweza kuwa na viwanja bora.

"Kuna timu zina uwezo wa kufanya vizuri uwanjani ila ajabu ni kwamba mazingira ambayo wanakutana nayo yanakuwa si rafiki, wanaanza kucheza kama wapo mchangani kumbe ni ligi.

"Ligi ina ushindani mkubwa kwani ila sasa tatizo ni ubovu wa miundombinu, viwanja bora bongo vichache, rafiki zangu kutoka nje wanaofuatilia ligi kupitia Azam TV, huwa wananihoji huko vipi mbona viwanja vyenu havina ubora? kuna kitu cha kufanya," amesema.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura amesema ni jambo la msingi kwa timu kuwa na uwanja wake hali itakayosaidia kusiwe na panguapangua ratiba hasa wenye viwanja wanapokuwa na matumizi yao binafsi.

"Tunaona kuna timu ambazo zimeanza kushughulikia utengenezaji wa miundombinu ya viwanja itasaidia kuimarisha ligi, hata Serikali kupitia kwa Waziri wa Habari ,Michezo, Sanaa na Utamaduni imezitaka timu kuwa na viwanja bora," amesema.

1 COMMENTS:

  1. Wambura acha majibu ya kiujanja ujanja wewe na bodi yako nyote ni mabomu mnapanguwa ratiba kwa kuzibeba timu na sio kwa sababu ya viwanja kwa kweli mmefeli hamna uwezo kabisa wa kuongoza ligi bora muache mkatafute kazi nyengine mfanye mko hapo kwa ajili ya kujaza matumbo yennu tu sio kuendeleza soka la Bongo kila siku linadidimia chini.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic