"Timu nyingi zinafanya vizuri na ushindani mkubwa unaonekana kwenye ligi na wengi wanapokutana na timu bora kama yetu wanaonyesha uwezo mkubwa," amesema.
Azam FC walipata sare mfululizo walianza na Biasahara United Uwanja wa Chamazi kisha wakalazimisha sare mbele ya Lipuli FC na jana walipoteza mbele ya Tanzania Prisons.
Wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 49 na vinara wa ligi ni Yanga baada ya kujikusanyia pointi 58.
Asante Azam kwa kuwa weledi waache kanda mbili waendelee kuwadangaja watu kuwa wanahjumiwa na kuacha eleza ukweli wa hali halisi ya ligi ilivyo. Vile tahadhari kwa Simba akija kuichukulia poa ligi kuu kitakajokutakumkuta asije akaja akaleta visingizio .
ReplyDelete