LEO uwanja wa Taifa kutakuwa na pambano la kukata na shoka ambalo litawakutanisha watani wa jadi, Simba na Yanga ikiwa ni mchezo wa marudio wa Ligi Kuu Bara.
Ikumbukwe kuwa mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa na Simba akiwa ni mwenyeji dakika 90 zilikamilika kwa suluhu ya bila kufungana, rekodi zinaonyesha kwamba mchezo wa Simba na Yanga huwa hauwaachi salama wachezaji kwani wengi walipata adhabu na kamati ya maadalili ya TFF ya masaa 72.
Mchezo uliopigwa Aprill 29/2018 uwanja wa Taifa wa msimu wa mwaka 2017/18 na Simba kuibuka kidedea kwa ushindi wa bao moja, beki wa Yanga Kelvin Yondani aliitwa na kamati ya masaa 72 iliyo chini ya Mwenyekiti Clement Sanga kwa kosa la kumtemea mate Asante Kwasi.
Pia Ofisa Habari wa Simba Haji Manara alipewa onyo kali na kamati ya masaa 72 kwa kosa la kuingia uwanjani kushangilia, Yodani alipuuzia kwenda kamati ya masaa 72 na hukumu yake iliisha kimyakimya akarejea Uwanjani.
Pia katika mchezo uliochezwa September 30/2018 ukiwa ni wa msimu wa 2018/19 na Simba ikiwa ni mwenyeji ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana, kamati ya masaa 72 iliwaweka kikaangoni wachezaji wawili wa Simba na Yanga.
James Kotei alipelekwa kamati ya masaa 72 kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Yanga, Gadiel Gabriel dakika ya 32 tukio ambalo mwamuzi hakuliona, pia Andrew Vincent wa Yanga alimpiga kichwa Mohamed Hussen 'Tshabalala' wa Simba na adhabu zao ilikuwa ni kufungiwa mechi tatu na faini ya milioni moja kwa kila mchezaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment