KOCHA mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kuwa amewaambia wachezaji wake leo watulie kwenye mchezo wao dhidi ya Simba utakaopigwa Uwanja wa Taifa.
Zahera amesema amewaandaa wachezaji wake kwa kuwapa mazoezi makali na mbinu mpya ambazo zitawasaidia kuibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa leo.
Zahera amesema hesabu ya kwanza ilikuwa ni kuwaweka sawa akili zao kisaikolojia ili wachukulie wepesi mchezo wao.
"Nimewapa wachezaji wangu zoezi maalumu linaloitwa kitaalamu 'Regenerarion' (Zoezi hili ni maalumu kwa ajili ya kuondoa stress kwa mwili). Pia nimewapa mazoezi ya mazoezi ya nadharia na vitendo. Zoezi lingine ni lile la misuli kwa wachezaji pamoja na zoezi la kupoteza mipira.
"Natambua utakuwa mchezo mgumu ila kila kitu kinawezekana wasidhani kama waliweza kufunga Al Ahly kwangu itakuwa rahisi, kuna tofauti kubwa kati yangu na Al Ahly," amesema Zahera.
Jambu kubwa lakunyanyuwa morali ya wachezaji ya wachezaji ni kurejea kundini kwa Kakolanya aliyekataliwa kwakudai haki zake na pia kuwapigania wachezaji kulopwa malimbiziko yao kwa sababu kuwajenga kisaykolojia pekeyake na huku wana njaa haitoshi na kusubiri bila mipaka kutazidi kubomowa.
ReplyDelete