February 9, 2019


Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Swed Nkwabi, amesema kuwa benchi la ufundi liliamua kumsajili Vitalis Mayanga ili kuziba nafasi ya Shiza Kichuya.

Hatua hiyo imekuja kufuatia mijadala mbalimbali iliyokuwa inatolewa na wapenzi, pamoja na mashabiki wa timu hiyo juu ya usajili wake.

Nkwabi ameamua kufafanua kwa kueleza Kocha Mkuu, Patrick Aussems, ndiye alipendekeza usajili wa Mayanga kuja Simba kuziba nafasi ya Kichuya.

Ikumbukwe Kichuya aliondoka Simba baada ya kukamilisha dili la kusajiliwa na klabu inayoshiriki Ligi Kuu Misri.

Kutokana na kuondoka kwake Simba ilianza kusaka mbadala wake na Mayanga kuoneakana kuwa anafaa na wanaamini ataitendea vema nafasi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic