February 9, 2019


BAADA ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Alliance katika Uwanja wa Chamazi, kikosi cha Azam FC kimeanza mazoezi jana jioni kwa ajili ya kuiwinda Lipuli ya Matola.

Kwenye mchezo wao dhidi ya Alliance dakika ya 79 katika mchezo uliochezwa jumatano kupitia kwa Joseph Mahundi walifunga bao la kuongoza  na katika dakika za lala salama Alliance walisawazisha kupitia kwa Dickson Ambundo.

Azam FC watacheza na Lipuli FC Uwanja wa Samora Februari 11, Iringa wakiwa na kumbukumbu ya kutoka suluhu kwenye mchezo wao wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Chamazi.

Azam wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wakiwa na pointi 48 baada ya kucheza michezo 21, huku Lipuli FC wapo nafasi ya nne baada ya kucheza michezo 24 wakiwa na pointi 36.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic