PATRICK Aussems, kocha wa Simba amesema kuwa hana hofu na safu yake ya ushambuliaji licha ya ubutu wanaokumbana nao wakiwa karibu na eneo la hatari.
Washambuliaji wa Simba wakiongozwa na John Bocco ambaye ni nahodha wamekuwa wakishindwa kutumia nafasi za wazi wakiwa eneo la hatari hali inayowafanya washindwe kupata mabao mengi kwenye michezo yao ya hivi karibuni.
Kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Ahly Bocco alikosa zaidi ya nafasi mbili za wazi pia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui alikosa nafasi tatu za wazi a kwenye mchezo dhidi ya Yanga licha ya kuingia kwenye box zaidi ya mara saba hakuleta hatari nyingi.
"Kwangu mimi sioni hatari washambuliaji kushindwa kufunga, inatokeoa kwenye mpira ila huwa ninawaambia wanapswa wawe makini, nitayafanyia kazi makosa yao hasa katika michezo yetu inayofuata," amesema.
Jana Simba walishinda bao 1-0 dhidi ya Yanga mchezo wa ligi kuu ambao unawafanya wafikishe pointi 39 na kurejea kwenye nafasi ya tatu.
Kimataifa we waache Simba wazembee tu wakati uwezo wa kuongeza fowadi wanao. .Muunganiko wa Juuko na wawa unaonekana kuimarika. Inaonekana Juuko taratibu anarudi kwenye uwezo wake unaofahamika huku Zana coulibali akiongezea kitu fulani kipya kwenye beki ya Simba. Hata Alahly usishangae ukisikia wanamfuatilia zana coulibali.Beki tatu bado hakujakaa vizuri shabalala anatakiwa kuongeza umakini zaidi na stamina. Shabalala anatakiwa kuongeza nguvu kwenye program zake za mazoezi hata chakula bado yupo mlaini na mwepesi mno. Bado safari ni ndefu Simba kunako club bingwa Africa na kama kweli wana malengo ya kusonga mbali zaidi na kama kweli wanayo nafasi ya kuongeza mchezaji kwa ajili ya mashindano hayo basi wahusika chonde chonde ongezeni fowadi mmoja wa nguvu. Inaonekana kuna udororo wa ufanisi kwa baadhi ya watendaji wa Simba huchukua maamuzi ya msingi kwa wakati. Angalia suala kocha msaidizi lilivyochukua muda yaani hatariii kama uharibifu tayari ulishafanyika, kwakweli wahusika wanatakiwa kubadilika. Hakika Boko yule tunayemfahamu sie kabisa huyu wa sasa na kila siku zikisonga mbele badala ya kuimprove anazidi kufifia nadhani anahitaji changamoto ya mchezaji mwengine mwenye uwezo zaidi yake labda atakijirekebisha la sivyo ukosaji umakini wake langoni mwa adui utaendelea kuitesa foward line ya Simba .
ReplyDeleteKOCHA NI VIZURI USIKILIZE USHAURI NA HOFU IWEPO ILI UTATUE HILO TATIZO MPIRA NI MAGOLI TUNATAKA SAFU YA WASHAMBULIAJI WAFANYIWE MAZOEZI MAALUMU YA UPACHIKAJI MAGOLI WAWE NA UWEZO WA KULENGA SHABAHA WAWE WEPESI WA KUPIGA MASHUTI WAWE NA SPIDI. WAPE ZOEZI LA KILA FOWADI KUPIGA MIPIRA YA KUPATA GOLI KWENYE LANGO LA WAPINZANI WAACHE KUUPANGA SANA MPIRA MPAKA WANAPOTEZA NAFASI
ReplyDeleteMfumo wa kocha hauwabebi baadhi ya wachezaji mfano huwezi kuwapanga okwi,kagere na bocco kwenye mechi moja ilitakiwa awe anawapanga okwi na bocco au okwi na kagere sasa unapowapanga wote unamnyima fursa okwi ya kucheza kwa Uhuru na pia mfumo wa sasa haumbebi chama ndio maana kiwango chake kimepungua
ReplyDelete